Full-Width Version (true/false)


Diamond: Hii ndio starehe yangu kubwa

Kila binadamu huwa na kitu ambacho hupenda kukifanya na akiwa anakifanya hukifurahia, wengine starehe yao ni kusoma vitabu, wengine kuangalia sinema, wengine kusikiliza muziki, wengine kunywa pombe na wengine starehe yao huwa ni kufanya kazi.
Sasa leo msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz amewaeleza mashabiki wake starehe yake kubwa ambapo kutokana na kazi yake wengi wangedhani hupendelea kwenda Club kuimba au kucheza muziki, au kunywa pombe na kadhalika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mara tu baada ya kuachia kibao chake cha Baila, Diamond amesema, kuwa kwenye mapenzi na kumpenda mtu ndio starehe yake kubwa.
Amesema mara nyingi watu maarufu hukutana na watu tofauti tofauti ambao wengine hupenda kweli, wengine hutamani kuwa na mtu huyo kutokana na umaarufu wake.
”Licha ya vingi vinipavyo furaha lakini kwenye mapenzi ama kumpenda mtu ndio starehe yangu kubwa na kama ujuavyo unapokuwa na kajina wengi wanakuwa wanakupenda, wengine kwa dhati wengine kwa matamanio”
Ameongezea ”Ila inapotokea anipendae nami nikampenda basi huyo hufaidi haswa mapenzi yangu, na ndio maana mara nyingi inakuwaga ni ngumu sana wengi kunisahau pindi tutenganapo, kwani huwaga na matendo mengi mazuri ya kimahaba yanayoonekana na yasiyoonekana gizani kwa sababu nayapenda mapenzi, na ni hodari sana kwenye kila taaluma ya kupetipeti.
Aidha Diamond Platinumz amesema amejifunza mengi sana katika mahusiano aliyowahi kuwa nayo.

No comments

Powered by Blogger.