Full-Width Version (true/false)


Exclusive: Muna afunguka “nitaanika kila kitu, ugonjwa wa Patrick mpaka kifo”

 
Mwanadada mjasiriamali Muna Love baada ya msiba wa mtoto wake kupita salama wiki iliyopita ameahidi kuzungumza kila kitu.

Mtumishi huyo wa Mungu ameiambia Bongo5 kwamba atazungumzia kuhusu ugonjwa wa mtoto wake, alivyoanza matibabu mpaka kifo chake pamoja na mambo mengine ambayo yalikuwa yanatokea.

“Nisikilizwe nachotaka kuongea toka mwanangu ameumwa mpaka kufariki sikuongea kitu,” Muna aliiambia Bongo5 “Ni watu tu walikuwa wanaongea na kunihukumu, wiki ijayo nitazungumza na waandishi kuweka sawa yote,”
Baada ya msiba huo kutokea mengi yalizungumzwa na watu huku kubwa zaidi likiwa ni lile la baba wa mtoto, Peter Komu kudai mtoto huyo alikuwa ni wake na sio wa Casto Dickson wa Clouds kama baadhi ya watu walivyokuwa wanadai.

Lakini kauli hiyo ilipingwa na mama wa mtoto huyo, Muna baada ya kutumia mtandao wake wa Instagram kueleza kwamba mtoto si wa Peter kama anavyodai bali niwa Casto kwani yeye ndiye aliyekuwa anajua kila kitu.

Mgogoro huo ulisabisha mvutano kati ya familia ya Muna naya Peter kuhusu msiba ufanyike wapi lakini baadaye wawili hao walikubaliana msiba ufanyike kwa Peter na ndipo ratiba ya mazishi ilivyoanza mpaka malaika huyo wa Mungu kuzikwa katika makabduri ya Kinondani jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.