Full-Width Version (true/false)


Fahamu majukumu na mkwanja wanaoingiza mameneja wa Diamond Platnumz kwa show moja

Kwa sasa ukitaja mameneja maarufu na wenye mafanikio makubwa kwa miaka mitano ya hivi karibuni kwa Afrika Mashariki kama sio barani Afrika, bila shaka huwezi kuacha kuwataja mameneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambao ni Babu Tale, Sallam na Mkubwa Fella.

Kutoka kushoto ni Babu Tale, Sallam, Diamond Platnumz na Mkubwa Fella.

Umaarufu wao haukuja kwa bahati mbaya bali ni kutokana na kazi kubwa za ubunifu wanazozifanya kila siku za kuhakikisha msanii wao Diamond anatoka hatua moja kwenda nyingine kimaendeleo na hilo halina ubishi kwani matokeo yake kila mmoja anayaona.

Diamond Platnumz anakuwa ni msanii wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na Mameneja watatu na wote tangu awe nao haijawahi kutokea tofauti yoyote ile kwenye utendaji kazi wao na kila siku anazidi kukua na kufanikiwa zaidi katika kazi yake ya muziki.

Unaweza ukajiuliza ni nini? haswa majukumu ya mameneja hao wote watatu?

Ni swali ambalo limekuwa likiwatatiza watu wengi hususani mashabiki wa Diamond Platnumz kuhusu utendaji kazi au majukumu ya kila meneja na hapa tumejaribu kuorodhesha majukumu yao.

i/Sallam.
Jukumu kubwa la Sallam kwa Diamond Platnumz ni kuangalia masuala ya biashara ya msanii huyo iwe ni Shows, Mauzo ya kazi zote za Diamond hapa ni kwenye mitandao na hard copy pamoja na kusimamia mikataba yake ya matangazo.

Sallam pia ndiye anayesimamia pia masuala yote ya kolabo na show zote za nje ya Tanzania anazofanya Diamond Platnumz.

ii/Babu Tale na Mkubwa Fela.
 Hawa majukumu yao wote karibia yanafanana na kazi yao kubwa kuangalia masuala ya Media sana sana Promosheni, ratiba za show na ushauri.

Ingawaje kila mmoja ana jukumu lake lakini hakuna meneja anayeweza kufanya maamuzi peke yake bali ni lazima washirikishane kwa pamoja tena mbele ya Boss wao Diamond Platnumz.

Ukirejea kwenye mahojiano aliyofanya Meneja Sallam mwaka 2016 na kituo cha Radio cha Swahili Talk cha nchini Denmark, alisema kuwa ingawaje kila mmoja ana jukumu lake katika kumuhudumia mteja wao, Diamond Platnumz lakini mameneja wote wanafanya kazi zao kwa ukaribu zaidi.

Je, mameneja hao watatu wanalipwaje na Diamond Platnumz?

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka WCB Wasafi mameneja hao watatu wanalipwa asilimia 30  ya kila show huku Diamond Platnumz akichukua asilimia 70 iliyobaki, malipo hayo ni ya show za nje na ndani.

Kwa sasa Diamond haijajulikana bado anatoza kiasi gani kwenye show zake za ndani hii ni kutokana na kukaa muda mrefu bila kutumbuiza nchini.

Diamond kwa show zote za nje anatumbuiza kwa dola $30,000 na kuendelea, hii inategemea na aina ya show na sehemu itakayotumika.

Kwa mahesabu rahisi ni kwamba show moja ya nje ya Diamond Platnumz ya bei ya chini ni dola $30,000 sawa na tsh milioni 68. Na ukiigawa katika asilimia Diamond atachukua milioni 47.6 ya 70% huku mameneja wake wakichukua milioni 20.5 ya 30%.

Hata hivyo bado haijajulikana ni kivipi mgawanyo wa mameneja hao unafanyika lakini kwa show ya nje Mameneja hao wanatengeneza si chini ya tsh milioni 20.

Hiyo ni kwa upande wa shows, kwa upande wa matangazo pia imeelezwa kuwa mgawanyo ni ule ule kama kwenye shows yaani 70% kwa 30%.

Asilimia hizo pia huenda kwa baadae Diamond Platnumz akaweza kuja kuzibadili kwani nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu wakati Diamond Platnumz anamtambulisha Mbosso WCB pale Hyatt Regency Hotel alikaririwa akisema “Kwa mara ya kwanza (Diamond Platnumz) kaleta mapinduzi kwetu sisi Mameneja kulipwa, wasanii wengine sisi ndio tunatoa hela lakini sisi huyu ndio anatulipa. 
Sallam analipwa, Mimi ni Diwani lakini nalipwa na huyu. Tale yule ana mishe mishe zake hapa mjini lakini analipwa na huyu. Mwanangu endelea kutulipa vizuri ndio nilichokuitia hapa (jukwaani ) sio kitu kingine“.

Hata hivyo, huenda Mameneja hao kwa sasa wanalipwa mkwanja mrefu zaidi ya hapo, hii ni kutokana na dili nyingi na kubwa anazozipata Diamond Platnumz kila siku kuzidi kuongezeka ikiwemo show kubwa za nje na ziara zake za muziki.

No comments

Powered by Blogger.