Full-Width Version (true/false)


Gigy Money afungukia kuhusu 'Lips' zake kaama amewahi kutumia sigara wala bangiMsanii wa bongo fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amesema hajawahi kutumia sigara wala bangi kama watu wanavyomfikilia kutokana na muonekano wake wa midomo inavyoonekana huku akidai kilichomuharibu ni utumiaji wa pombe kali. 

Gigy Money ameeleza hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv baada ya kuwepo tetesi zinazosambaza kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha msanii huyo kujihusisha na matumizi ya uvutaji wa bangi na sigara kutokana na midomo yake kuwa meusi.

"Sijawahi kutumia bangi, sigara na wala sijui dawa za kulevya jinsi zilivyo hata sizifahamu, mimi ni 'Gigy by natural' jamani, na situmii hayo wanayosema kama vipi wanifungie kwenye nyumba tukae halafu waone kama nitabadilika", amesema Gigy.

Pamoja na hayo, Gigy ameendelea kwa kusema "waende wakamuangalia mama yangu midomo yake jinsi ilivyo, sisi ni walevi. Midomo imeshaungua na konyagi na vitu vingine vingi, sasa mnataka mtu asinywe pombe kwa sababu 'lips' zitaharibika".

No comments

Powered by Blogger.