Full-Width Version (true/false)


“Hairuhusiwi kupigwa faini mara 2 kwa kosa 1”-Polisi


Leo July 10, 2018 tunayo story kutokea kwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Victor Ayo ambaye ni Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Kipolisi Temeke, ambapo amesema Askari atakayempiga faini dereva mara mbili kwa kosa moja atamchukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.

Mrakibu Ayo ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa madereva wa malori ya Mchanga na Mawe Maweni Kigamboni ambapo amesema amewabaini wana uzembe barabarani.

Amesema endapo akibaini kuna Askari amemtoza faini dereva mara mbili katika kosa moja atamfukuza kazi.

“Faini ya kosa moja lina dumu kwa saa 24 na lengo ni kutaka dereva ajutie na kujirekebisha, sasa ukimpiga faini kwa kosa hilo hilo ndani ya muda mfupi huo sio utaratibu mzuri, “ Mrakibu Victor Ayo

Pia Mrakibu Ayo, amesema hatua ya kutoa elimu kwa madereva hao inatokana na kubaini uzembe miongoni mwa madereva hao ambapo wengi wanasababisha ajali kutokana na kujiamini kwa ukubwa wa magari yao.

No comments

Powered by Blogger.