Full-Width Version (true/false)


Hatimaye Watoto 12 na Mwalimu wao wameokolewa ThailandLeo July 10, 2018 kutoka nchini Thailand Watoto 12 pamoja na Mwalimu wao wa mpira wa miguu ambao walikuwa wamekwama kwenye pango lililokumbwa na mafuriko wameokolewa.

Watoto hao walikwama June 23 walianza kuokolewa kwa makundi na hatimaye mchana huu kundi la mwisho limefanikiwa kutoka ndani ya pango hilo.

Watoto 8 waliokolewa siku ya Jumapili na Jumatatu huku wakiwa na afya njema ya akili na mwili, Wanajeshi wa Kikosi cha Maji walifanikiwa kuwapelekea chakula mara baada ya kutambua umbali waliopo kabla ya juhudi za uokozi kuanza.

Watoto hao walikwama umbali wa Kilomita 4 kutoka kwenye mdomo wa pango hilo. Siku ya Ijumaa Mwanajeshi mmoja wa kikosi cha uokoaji alifariki dunia kwa kuishiwa na hewa ya Oksijeni wakati akiwa kwenye harakati za zoezi la uokoaji.

No comments

Powered by Blogger.