Full-Width Version (true/false)


Hawa hapa watakaoikosa safari ya Yanga kuelekea Kenya leo, sababu zatajwa


Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuondoka nchini leo, baadhi ya wachezaji hawatakosekana katika msafara wa timu hiyo.

Hassan Kessy pamoja na beki Kelvin Yondani ndiyo wachezaji pekee watakaobaki Dar es Salaam kutokana ambao wameelezwa hawakuwa kambini na Yanga.

Kwa mujibu kwa Ofisa Msaidizi wa Habari Yanga, Godlisten Chicharito , amesema Kessy na Yondani hawakuwa kwenye ratiba ya mazoezi na Kocha Mwinyi Zahera hivyo hawatoambtana na timu kuelekea Kenya.

Awali ilielezwa kuwa Yondani na Kessy wamegoma kusafiri na timu ikielezwa wanashinikiza kuongezewa mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga lakini uongozi umeibuka na kueleza tofauti.
Aidha, wachezaji Heritier Makambo, Mrisho Ngassa na Deus Kaseke waliosajiliwa hivi siku kadhaa zilizopita hawatokokuwa sehemu ya kikosi dhidi ya Gor Mahia kutokana na majina yao kuchelewa kuwasilishwa CAF.

Yanga itaondoka leo tayari kuikabili Gor Mahia katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Nairobi siku ya Jumatano, Julai 18 2018.

No comments

Powered by Blogger.