Full-Width Version (true/false)


Hawa: "Pombe Nayo ni Madawa ya Kulevya, Mimi ni Muathirika wa Pombe za Kienyeji'

Mwanadada Hawa ambae aliwahi kuwika sana kipindi cha nyuma kutokana na kushirikishwa katika wimbo wa Diamond amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa hawajui kama hata pombe pia  inaweza kumfanya mtu kuharibikiwa kama madawa ya kulevya.

Hawa ambae alikuwa muathiika wa pombe zakienyeji kwa muda mrefu na kuuua kabisa kipaji chake cha muziki mpaka pale alipopata watu wa kumsaidia anasema kuwa haikuwa rahisi kwake kutoka huko kama asingepatiwa msaada kama wanavyowatokea waathirika wa madawa ya kulevya.

"Pombe pia ni miongoni mwa madawa ya kulevya sema tu watu wamekuwa hawalijui hilo,maana mimi pia ni muathurika wa pombe"

Hata hivyo mwanadada huyo ambae kwa sasa hali yake imeanza kuimarika, anasema kuwa anajipanga upya na kuja kivingine ili kuendeleza kipaji chake cha muziki kwa kuwa anaamini kipaji anacho.

No comments

Powered by Blogger.