Full-Width Version (true/false)


Hii ndio sababu Diamond kufanya kama Shahrukh Khan video ya ‘Baila’Kufuatia kuachiwa kwa wimbo mpya wa Diamond Platinumz ”Baila” umezua mijadala mingi mitandaoni, wengi wemesema baadhi ya vipande vya video katika wimbo huo vimeigwa toka kwa msanii maarufu nchini India Shahrukh Khan aliyepata umaarufu wake hapa nchini kwa sinema yake ya kuchi-kuchi Hotae.
Saa moja iliyopita Diamond Platinumz kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe mfupi unaoweza kujibu mijadala hiyo iliyozuka mtandaoni.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika.
”Sababu kubwa ya kumpenda Shahrukh Khan sio tu kuigiza bali ni ufundi na kubobea kwake kwenye sekta ya uigizaji wa mapenzi katika movie zake”.
Ambapo tayari kurasa mbalimbali za watu huko Instagram wamekata kipande ambacho Diamond ameonekana kuiga toka kwa msanii huyo Shurkhan na kukilinganisha.
Hata hivyo siku chache zilizopita msanii huyo, Diamond aliweka bayana kati ya watu anaowakubali katika maisha yake yaani ”RoleModels”  alimtaja Shahrukh Khan  ambaye alionekana kushika namba mbili kati ya waigizaji filamu tajiri nchini India ambaye kipato chake ni dola za kimarekani 740.

No comments

Powered by Blogger.