Full-Width Version (true/false)


Hii ndio sababu ya Masanja kuokoka

Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’

Aliyekuwa mchekeshaji wa Kundi la ‘Ze Comedy’ Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ambaye kwa sasa ni mshereheshaji na mchungaji, ameibuka na kusema kuwa kuogopa kifo ndio sababu iliyomfanya aokoke.

Masanja ambaye pia ni baba wa mtoto mmoja aliyasema hayo hivi karibuni mara baada ya kukutana na paparazzi wetu katika harakati za kuuaga mwili wa mtoto wa Muigizaji wa Filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’ aitwaye Patrick maeneo ya Leaders, Kinondoni jijini, Dar.

Msanii huyo alisema kuwa, aliokoka kwa sababu ya kuogopa kifo na kwamba katika vitu ambavyo hapendi kuvisikia katika maisha yake ni habari zinazohusiana na kifo kwani huingia woga sana.

“Niliokoka kwa sababu ya kuogopa kifo na mtu akitaka tugombane azungumzie habari za kufakufa yaani huwa sipendi hata kuzisikia natamani kuishi tu na kwasababu ninaimani ukimfuata Yesu unakuwa mikono salama ndio maana nimechagua njia hiyo,” alisema Masanja.

No comments

Powered by Blogger.