Full-Width Version (true/false)


Hii ndio timu aliyojiunga nayo Obrey Chirwa wa Yanga

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, amejiunga na club mpya ya Misri aliyojiunga nayo kama mchezaji huru.

Chirwa amethibitishwa rasmi kujiunga na club ya Nogoom El Mostakbal Football Club ya Ligi daraja la pili Misri, club hiyo imeanzishwa miaka 12 iliyopita na mafanikio yake makubwa ni kucheza Egypt Cup na kutolewa na Zamalek.

Taarifa za Chirwa kujiunga na club hiyo zimetolewa rasmi kupitia ukurasa wa instagram wa club hiyo “Tuna furaha kumtambulisha mshambuliaji mpya Obrey  Chirwa ambaye nimchezaji wa zamani wa club ya Yanga ya Tanzania”

No comments

Powered by Blogger.