IGP aingia kwenye 18 za Waziri Lugola

Waziri
Lugola ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika
makao makuu ya kikosi cha kutuliza ghasia kilichopo Ukonga Jijini Dar es
Salaam na kuongea na Askari wa Kikosi hicho na wale wanaohudumia katika
uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
Wakati akitoa agizo hilo, Mhe. Lugola
amesema kuwa ili kufikia Uchumi wa kati Watanzania wanatakiwa kufanya
kazi za kiuchumi kwa masaa 24 hivyo IGP anapaswa kumhakikishia mikakati
ya jeshi lake katika ushiriki wao wa kuwapatia watanzania usalama kwa
muda wotewakifanya shughuli hizo za kiuchumi.
"Nataka IGP aje aniambie kwamba je,
jeshi la polisi limesalimu amri kwa majambazi ndiyo maana mabasi
hayatembei usiku, lakini biashara mbalimbali ikifika saa 12 zinafungwa,
ukiuliza unaambiwa ni kwa sababu ya usalama, nataka IGP aniambie kama
majambazi ndio wanaotupatia amri...Hatuwezi kukubali kupewa amri na
majambazi ni masaa mangapi tunatakiwa kuganya shughuli za kiuchumi au
kupangiwa maeneo ya kwenda na wapi tusiende," Waziri Lugol
No comments