Full-Width Version (true/false)


Jafo ataka wafanyakazi nchini kuwekeza kwenye Korosho


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo ameviagiza vyama vya wafanyakazi nchini kutumia sehemu ya michango inayochangwa na wanachama wake ipelekwe katika uwekezaji wa viwanda hususani viwanda vya Korosho na Alizeti badala ya kuendekeza migogoro isyo na tija rushwa na kugombania vyeo.

Akizungumza wakati akizindua zoezi la uuzaji wa hisa za chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU uliofanyika jijini Dodoma Waziri Jafo amesema wakati huu Tanzania ikielekea katika uchumi wa viwanda kuna kila sababu ya vyama vya wafanyakazi kuunga mkono juhudi hizo katika uwekezaji wa viwanda.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU taifa Bw.Suleiman Kikingo amesema kuuzwa kwa hisa hizo itakuwa ni chanzo cha kuwasaidia watumishi na kuwakwamua kutoka katika hali duni za maisha

No comments

Powered by Blogger.