Full-Width Version (true/false)


Jumuiya ya Vijana CUF watolea ufafanuzi kuhusu kuvuliwa Uanachama Madiwani watatu
Jumuiya ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF wilaya za Dar es Salaam wametolea ufafanuzi taarifa za kuvuliwa uanachama kwa Madiwani watatu wa chama hicho mkoani Tanga.


 Madiwani hao waliovuliwa uanachama ni diwani wa kata ya Mwanzange na Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya ya Tanga, Rashird Jumbe pamoja na wenzake wawili wa viti maalum, Halima Juma na Fatuma Maine.


 Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilaya ya Ilala, Canaly Kitimai alisema wameamua kutolea ufafanuzi wa taarifa hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa za uzushi zinazotolewa na Julius Mtatiro.

 " Tumesoma andiko la Mtatiro facebook kwamba kitendo cha kuwafukuza madiwani hawa kwamba Mwenyekiti Lipumba na Kaimu Katibu Mkuu, Sakaya wanashiriki kudhoofisha chama, tunaweka kumbukumbu sawa kuwa maamuzi haya siyo ya Mwenyekiti bali ni ya Baraza Kuu kwa mujibu wa katiba yetu.


 " Malengo ya chama cha siasa ni kushinda chaguzi sasa kitendo cha Mtatiro kusema hawatoshiriki uchaguzi ni uhuni ambao sisi hatuwezi kuuvumilia," Amesema Canaly.


 Amesema msimamo wao ni kuunga mkono maamuzi sahihi ya baraza kuu kuwavua uanachama Madiwani hao na kumdharau Mtatiro na genge lake ambalo wanashinda mitandaoni kwa lengo la kudhoofisha.


" Kwa kuwa Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeshindwa kuchukua hatua za kisheria za kumdhibiti kibaraka Mtatiro sisi Vijana tutamdhibiti kwa nguvu zote kibaraka huyu wa Chadema ," amesema.


No comments

Powered by Blogger.