Full-Width Version (true/false)


JWTZ waanzisha mpango wa kuwaandikisha jeshini wanafunzi
Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania  JWTZ kupitia shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi ya RTS Kihangaiko limeanza kutekeleza mpango maalum wa kuwaandikisha  jeshini moja kwa moja kutoka shuleni wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufanya vizuri kwenye masomo ya sayansi lengo likiwa ni Tanzania  kupata askari wasomi wenye uwezo mkubwa wa kiteknolojia watakaoweza kukabiliana na wahalifu na ugaidi wenye teknolojia ya juu ambao unaendelea kwa kasi kubwa duniani


Mkuu wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi  RTS Kihangaiko Kanali Sijaona Myala ametoa kauli hiyo  katika hitimisho la mafunzo  ya matumizi ya silaha za kivita  kwa askari  wanafunzi  zaidi ya mia nne yaliyofanyika katika  eneo la vilima saba Msata wilayani Bagamoyo.


Mkuu wa mafunzo ya kivita  makao makuu ya jeshi la  ulinzi la wananchi  wa Tanzania Brigedia Generali Deodatus Kanyata anasema jeshi lina wajibu mkubwa wa kuhakikisha rasilimali zote za nchi zinakuwa salama  wakati wote kwa manufaa ya taifa hivyo kuna muhimu wa kuwa na jeshi la kisasa lenye wasomi.


Wakufunzi wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi ya RTS Kihangaiko nao wapata nafasi ya kutoa nasaha ka vijana wanaojiunga na jeshi hilo.

No comments

Powered by Blogger.