Full-Width Version (true/false)


Kenyatta afanya mabadiliko, mwanamke amkosha


Rais Uhuru Kenyatta leo amemteua na kumtangaza Meja Jenerali Fatuma Ahmed kuwa  Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi katika kitengo cha kusimamia wafanyakazi na vifaa na uchukuzi. 
Meja. Fatuma anakuwa Mwanamke wa kwanza nchini Kenya kushika nafasi hiyo ya juu ndani ya Jeshi la nchi hiyo huku Kenyatta akivunja rekodi kwa kuwa Rais wa kwanza kumteua mwanamke wa kwanza kwenye wadhifa huo.

"Ni furaha yangu kuwa Rais wa kwanza kumteua mwanamke wa kwanza kwenye wadhifa wa juu katika uongozi wa jeshi la taifa letu la Kenya, Meja Jenerali Fatuma Ahmed kama msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akisimamia wafanyakazi na vifaa na uchukuzi," Kenyatta. 

Hii inakuwa mara ya pili kwa Meja. Fatuma Ahmed kuingia kwenye historia ya kuchaguliwa kwenye nafasi nyeti kwani miaka mitatu iliyopita, alichaguliwa kuwa Brigedia mwanamke wa kwanza nchini Kenya.

"Ninakuhesabu kuwa mfano mzuri kwa wanawake wengine katika Jamhuri hii...Unachopaswa ni kuwahakikishia kwamba hakuna kikomo kwa wanawake wa Kenya na kwamba kila kitu kinawezekana," Kenyatta amesema.

Katika uteuzi huo wa Rais Kenyatta uliofanyika leo ni pamoja na Luteni Jenerali, Robert Kibochi kuwa Makamu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Kenya ambaye amechukua nafasi ya Luteni Jenerali, Joseph Kasaon baada ya kustaafu, Luteni Jenerali, Raria Koipaton kuwa Kamanda wa Jeshi la Kenya na Meja Jenerali, Francis Ogolla kuwa Kamanda wa Jeshi la anga la Kenya.


Rais Uhuru Kenyatta akiwa na viongozi wa Majeshi aliowateua siku ya leo Ijumaa ya Julai 13.

No comments

Powered by Blogger.