Kiongozi mkubwa wa upinzani aahidi kubadilisha jina la nchi, adai jina la sasa lina laana

Kiongozi huyo akimwaga sera kwenye kampeni za kuwania Urais nchini humo Jana Julai 16, 2018 mjini Mutare amesema kuwa jina la taifa hilo limelaaniwa na ndio maana taifa hilo limekuwa nyuma kwenye kila kitu.
“Jina la Zimbabwe limelaaniwa hatuwezi tena kutumia jina hilo kwenye utawala wangu kama mtanipatia kura. Oneni wenyewe nchi yetu ilivyogeuzwa kuwa pagale na kila mtu duniani akiipatia picha mbaya, hatuwezi kubaki na hili jina tutakuwa tunaishi na laana iliyodumu kwa miaka mingi, mimi naiona Great Zimbabwe kwenye utawala wangu,“amesema Chamisa.
Chamisa ni kiongozi pekee wa vyama vya upinzani mwenye ushawishi zaidi kwenye uchaguzi mkuu wa urais nchini Zimbabwe unaotarajiwa kufanyika Julai 30, 2018 ambapo Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa atapambana naye kupitia tiketi ya chama tawala cha ZANU-PF.
Chamisa alichukua nafasi ya kuwa kiongozi mkubwa wa chama chenye nguvu cha Upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC) baada ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Morgan Tsvangirai .
Hata hivyo Zimbabwe kubadilisha jina lake haitakuwa stori kubwa kwani miaka ya nyuma kabla ya 1960 taifa hilo lilikuwa linaitwa Southern Rhodesia kabla ya kuitwa Zimbabwe jina linalotokana na maneno mawili “DIZIMBA” na “DZAMABWE” yenye maana ya nyumba ya mawe kwa lugha ya Shona inayozungumzwa na watu wengi nchini Zimbabwe kwa sasa.
No comments