Full-Width Version (true/false)


Kocha mpya Simba hana habari na Yanga

Dar es Salaam. Kocha Mpya wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amesema hana habari na watani zao wa jadi Yanga, yeye mipango yake ni kuifanya Simba kuwa big team Afrika.
Patrick amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa klabi hiyo huku akisisitiza kuwa atafanya Kazi na makocha wazawa.
Katika hafla ya kumtambulisha kocha huyo alisema anaijua Yanga na Azam lakini Simba ndiyo kila kwake.
"Kama nilivyosema naifikiria Simba kuwa moja ya timu kubwa Afrika, tageti yangu ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufika mbali mashindano ya kimataifa," alisema.
Rais wa Simba, Salim Abdallah alisema wamempa mkataba wa mwaka mmoja na atafanya Kazi akisaidiana na Masudi Djuma sanjari na Kocha wa viungo ambaye atatajwa siku si nyingi.

No comments

Powered by Blogger.