Full-Width Version (true/false)


Kocha Zahera kuishuhudia Yanga ikicheza na Gor mahia leo akiwa jukwaani, sababu ni hii

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, leo atakosekana katika benchi la ufundi la timu yake kutokana na kukosa vibali vya kufanyia kazi.Zahera amekuwa akiinoa Yanga tangu achukue mikoba ya Mzambia, George Lwandamina, lakini mpaka sasa hajapatiwa vibali kitu ambacho kinamfanya aendelee kukosekana kwenye benchi la ufundi.Taarifa kutoka kwa viongozi wa Yanga zinasema uongozi mpaka sasa unapambana kuhakikisha unapata vibali kwa ajili ya Zahera ili kuweza kutimiza majukumu yake kama Kocha kwa asilimia 100.Yanga itakuwa inashuka dimbani leo kucheza mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Gor Mahia FC wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Zahera atakuwa jukwaani.Kuelekea mechi hiyo tayari Zahera ameshakiandaa kikosi hicho ambacho kitaongozwa na Noel Mwandila kusukuma gozi dhidi ya wapinzani wao ambao mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini Kenya

No comments

Powered by Blogger.