Full-Width Version (true/false)


Kombe la Dunia 2022 Qatar kupigwa Desemba

 

Moscow, Russia. Shirikisho la soka la kimataifa (Fifa), limetangaza rasmi fainali za Kombe la Dunia 2022 Doha nchini Qatar, zitafanyika kati ya Novemba 21 na Desemba 18.

Hii ni mara ya kwanza kwa fainali za Kombe la Dunia, kufanyika miezi ya mwishoni mwa mwaka.

“Uamuzi wa mwisho ulihusu tarehe ya kuchezwa Kombe la Dunia 2022 umefanyika, itafanyika nchini Qatar kati ya Novemba 21 na Desemba 18, 2022,” alisema Rais wa Fifa, Gianni Infantino.

Alisema kamati ya utendaji imefanya uamuzi huo kwa kuzingatia hali ya hewa ya Qatar ambako katika miezi Juni na Julai kunakuwa na joto kali ambalo haliruhusu mechi za ushindani kufanyika.

Alibainisha kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Fifa na taasisi nyingine zikiwemo za afya, umethibisha kuwa miezi hiyo hakutakua na joto la kudhuru kama ambavyo ingekua Juni na Julai.

Aidha alisema fainali za mwaka 2022 zitaendelea kushirikisha timu 32 kama desturi ilivyo isipokua kuanzia zile za 2026 zitakazofanyika katika nchi tatu tofauti Marekani, Mexico na Canada, zitashirikisha nchi 48.

Alisema katika fainali za 2026 ndipo watakapotangaza nchi mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2030.

No comments

Powered by Blogger.