Full-Width Version (true/false)


Kuhusu vitambulisho vya Taifa visivyo na sahihiMamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa suala la kubadilisha vitambulisho vya awali ni gharama kwa serikali hivyo wameamua kutafuta njia mbadala ambayo imeanza kutekelezeka bila kuathiri upatikanaji wa taarifa za mhusika.
 
 
Akizungumza na eatv. Mkuu wa kitengo cha mawasiliano NIDA, Rose Mdami, amesema kuwa mamlaka imeelekeza vitambulisho vyote vitumike na endapo zoezi la kubadili vitambulisho litafanyika, itakuwa baadaye baada ya kukamilisha usajili nchi nzima.

Zoezi la kubadili vitambulisho vya awali kama litafanyika ni baadaye sana, kwani zoezi hilo litagharimu fedha kwa mantiki hiyo tunapunguza gharama kwa serikali na tumeunda kitu kinachoitwa tovuti salama ambayo itakayomsaidia mtu kutumia kitambulisho cha awali na taarifa zake zikaonekana na tovuti hii inaweza kutumiwa na mamlaka zote zitakazo hitaji taarifa za mhusika”, amesema Mdami.

Hayo yanajiri ikiwa  ni  miaka miwili  tangu  kutoka  kwa  tamko  la  Rais  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tazaniana  Dkt.  John  Pombe  Joseph  Magufuli  kuitaka  Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA)  kuhakikisha  inabadilisha  vitambulisho  kwa  kila  mwananchi  kutokana na vitambulisho vya awali kukosa sahihi ya mmiliki.

No comments

Powered by Blogger.