Full-Width Version (true/false)


Kwa mziki huu: ubingwa Simba mapemaa


Straika wa timu ya Simba, Marcel Kaheza ambaye amesajiliwa akitokea timu ya Majimaji kwa thamani ya shilingi milioni 30, amesema kuwa vita ya ubingwa wa Kombe la Kagame itamalizika mapema tu kwa kuwa wamejipanga kuhakikisha wanabeba kombe hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Kaheza amesema kuwa katika michuano hiyo ushindani umekuwa mkubwa, hivyo wamejipanga kuhakisha kwamba wanawapa mashabiki kile ambacho wanakihitaji ambacho ni ubingwa.

“Thamani ya mchezaji ni kuweza kufanya vizuri uwanjani na ushindani uliopo ni lazima kupambana hivyo kazi kubwa ni kuweza kupata matokeo mazuri ambayo yatasaidia timu kuibuka na ushindi hali itakayoongeza furaha kwa mashabiki na uongozi wa timu.

“Timu ipo vizuri kwa kuwa wachezaji wote tunajua kazi yetu na tutashirikiana katika kuhakikisha tunapata ushindi kwa kuwa tunacheza tukiwa ni timu malengo yetu yanafanana, hakuna kitakachoharibika tunashirikiana vizuri na wachezaji wote, mashabiki watupe sapoti,” alisema Kaheza.

Timu ya Simba imefanikiwa kubeba ubingwa wa Kombe la Kagame mara sita huku Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wakiwa wamefanikiwa kuchukua ubingwa huo mara moja mwaka 2015.

No comments

Powered by Blogger.