Lowassa, Zitto Kabwe Wakutana Faragha
Waziri
Mkuu wa zamani Edward Lowassa na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo,
Zitto Kabwe wamekutaka na kufanya mazungumzo leo Alhamisi Julai 19,
2018.
Taarifa
iliyotolewa leo na msaidizi wa waziri mkuu huyo, Aboubakary Liongo
imesema katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwa Lowassa,
viongozi hao walijadiliana juu ya mwenendo wa hali ya siasa Tanzania na
mchango wa vyama vya siasa kwenye maendeleo ya nchi.
Taarifa
hiyo iliyoambatana na picha zinazowaonyesha wawili hao wakijadiliana
masuala mbalimbali, haikueleza kiundani walichozungumza.
No comments