Full-Width Version (true/false)


Maandamano kupinga kodi ya matumizi ya mitandao ya kijamii yazuiliwa Uganda


KAMPALA, UGANDA
POLISI Uganda wamesema hawataruhusu maandamano yaliyopangwa dhidi ya kodi iliyotangazwa hivi karibuni na serikali kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii na huduma za kutuma pesa kwa simu za mkononi nchini humo.

Msemaji wa Polisi Emilian Kayima amesema waandaaji wa maandamano yaliyopangwa kufanyika kesho hawajaomba ruhusa ya polisi kwa mujibu wa sheria.

Kayima pia alisema, hakuna mtu aliyetoa ombi kama inavyoagizwa na sheria.

Wanaharakati wakiwemo wabunge wa upinzani, wasanii na mashirika ya kijamii wameutaka umma kujitokeza mjini Kampala kupinga kodi ya kila siku ya dola 0.05 za kimarekani kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii na ushuru wa asilimia 0.5 kwa miamala za kutuma na kupokea pesa kupitia simu za mkononi.CRI

No comments

Powered by Blogger.