Full-Width Version (true/false)


Mabasi yatakayochezea kifaa cha kudhibiti mwendo kufungiwa huduma zakeKamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Fortunatus Muslim amewaagiza wamiliki wa mabasi yanayokwenda mikoani kuhakisha wanafunga vifaa vya kudhibiti mwendo kasi ili kupunguza ajali na kama kuna basi litakalobainika kutofunga ama limefunga lakini kifaa hicho kimechezewa basi hilo litafungiwa kutoa huduma. 

Kamanda Muslim ameysema hayo alipokutana na wamiliki wa mabasi hayo kuweka mkakati wa namna ya Kudhibiti ajali hizo. Kwa upande wake katibu wa chama cha wamiliki wa mabasi nchini Bw.Ernea Mrutu amesema wamekubaliana mambombalimbali ikiwemo kuhakisha kuwa magari yao wanayatengeneza mara kwa mara na kuhakisha kuwa waajiri Madereva wenye vigezo.

No comments

Powered by Blogger.