Full-Width Version (true/false)


Mabingwa Simba waongoza kwa mapato ya mlangoni, hata hivyo bado ni kiduchuMabingwa wa soka Tanzania, Simba ndiyo timu iliyoingiza fedha nyingi zaidi katika viingilio vya mlangoni wakati wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017-18.

Katika mechi 30 ilizocheza, Simba imefanikiwa kuingiza kitita cha Sh milioni 380.8 ikifuatiwa na Yanga yenye milioni 257.2.

Hata hivyo, pamoja na fedha hizo ambazo wanaonekana kuingiza watani hao kwa msimu mzima, inaonyesha mapato ya mlangoni yameporomoka kwa kiasi kikubwa sana.

Kama utagawanya kwa mzunguko mmoja wa mechi 15, maana yake Simba iliingiza Sh milioni 190 tu ambacho ni kiwango cha chini zaidi.MAPATO YA MLANGONI LIGI KUU BARA 2017-18
1. Simba      380,867,592
2. Yanga      257,113,365

No comments

Powered by Blogger.