Full-Width Version (true/false)


Magufuli kuwaapisha balozi Sokoine, kamishna jenerali wa Magereza.
Rais John Magufuli leo Jumamosi Julai 14, 2018 atawaapisha Balozi Joseph Sokoine kuwa Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Phaustine  Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema Kasike aliteuliwa jana Julai 13, 2018 na Balozi  Sokoine aliteuliwa Julai Mosi, 2018.
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao itafanyika leo Julai 14 katika ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam kuanzia saa 9:00 alasiri.


No comments

Powered by Blogger.