Full-Width Version (true/false)


Maiti Yazungumza Kabla ya Kuzikwa..Yamtaja Aliyemtoa KafaraMACHAKOS. Watu wengi waliohudhuria mazishi walisalia vinywa wazi kusikia sauti kutoka kaburini, baada ya mwili wa msichana mmoja aliyekuwa kafariki katika ajali ya barabarani kumtaja mjomba wake kuwa ndiye aliyetumia kafara kumuua ili atajirike

Maeneo ya Masii, Machakos nchini Kenya, kilizuka kioja katika mazishi ya mwanadada huyo aliyefariki katika ajali ya barabarani. Inadaiwa kuwa mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa akiishi na mjomba wake mjini Voi kabla ya kifo chake.

Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika gazeti la “Taifa Leo” la nchini humo, mwanadada huyo alifariki katika ajali ya barabarani na mwili wake kupelekwa katika mochwari ya eneo hilo na kwa muda wa mwezi mmoja mwili haukutambuliwa wala hakuna ndugu yeyote aliyejitokeza hapo.

Baadae wahudumu wa mochari hiyo waligundua baada ya mwezi mmoja kuwa maiti huyo alikuwa na kitambulisho mfukoni mwake, walitumia kitambulisho hicho kuwatafuta jamaa wake.

Limekuwa ni jambo la kustaajabisha wengi hasa majirani na ndugu zake huyo binti kwa sababu mjomba aliyekuwa akiishi na msichana huyo hakutoa habari zozote kuhusu kutoweka kwa msichana huyo.

“Licha ya kukosa kurudi nyumbani na kuwasiliana naye, mjomba hakushugulika kujua aliko hadi polisi walipowasiliana na familia yake,” Mmoja wa watu waliokuwa msibani aliongezea.

Watu walisalia kimya hadi siku ya mazishi huku kioja kikizuka wazi. Shuguli ya mazishi ilipoanza waombolezaji walishangazwa na sauti iliyokuwa ikitoka kaburini. Maiti alianza kuzungumza huku akieleza jinsi mjombake alivyopanga kifo chake kwa kutumia ndumba ili apate mali.

Alisema kuwa alikuwa ametolewa kafara jambo lililopelekea hasira kupanda kwa waombolezaji na kutaka kumvamia mjomba huyo, ijapo maafisa wa polisi walifika hapo upesi na kumuokoa.

No comments

Powered by Blogger.