Full-Width Version (true/false)


Makonda aeleza mafanikio ya Serikali katika mkoa wa Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Julai 14, 2018 ameandaa mkutano wa kuwaelezea wananchi na Viongozi wa Chama cha mapinduzi (CCM) kuhusu miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kupitia Serikali ya awamu ya tano kwenye Mkoa wa Dar es salaam chini ya Ilani ya CCM inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Makonda amesema kwa kipindi cha muda mfupi Serikali ya CCM imefanya mapinduzi makubwa kwenye Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Miundombinu, Umeme, Maji, Ulinzi na Usalama, Usafiri na ujenzi wa Viwanda.


Kuhusu sekta ya elimu Makonda amesema Serikali imefanikiwa kutoa elimu Bure, ujenzi na ukarabari wa madarasa, ununuzi wa madawati, ujenzi wa shule mpya,ujenzi wa Hostel, mabweni pamoja na ujenzi wa ofisi 402 za walimu ambapo zipo zilizokamilika na nyingine zipo hatua ya mwisho kukamilika.
Aidha, Makonda amesema Serikali kwa kushirikisha wadau imefanikisha ujenzi wa Jengo la Mama na mtoto hospital ya Chanika, Amana, Jengo la Upasuaji Mwanayamala, jengo la wagonjwa wa dharura Temeke, Zoezi la upimaji afya Bure kila mwaka, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya pamoja na kusimamia upatikanaji wa dawa, vifaa tiba pamoja na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.


Kwa upande wa Sekta ya miundombinu ya barabara, Makonda amesema Serikali imefanikiwa kujenga barabara,mifereji na madaraja kupitia miradi iliyopo chini ya TANROAD, TARURA na DMDP jambo lililosaidia kupunguza kero kwa watumiaji wa barabara.
Pamoja na hayo, Makonda ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. Magufuli imefanikiwa kuboresha mazingira ya kazi kwa jeshi la Polisi kupitia ujenzi na ukarabati wa vituo vya polisi, kuwapatia magari, pikipiki, baiskeli na compyuta na kufanya polisi kuwa na morali ya kazi na kupungua kwa uhalifu.
Amesema sekta nyingine ambazo zimetekelezwa kwa mkoa wa Dar es salaam kupitia ilani ya CCM ni pamoja na utawala bora, uchumi, kilimo, maji, kilimo, maliasili na utalii, mazingira, usafirishaji.

No comments

Powered by Blogger.