Full-Width Version (true/false)


Manara atoa msimamo kuhusu kambi ya Simba


Kuelekea ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2018/19, kambi ya mabingwa watetezi Simba, imeendelea kuwa siri licha ya wachezaji waliokuwa mapumzikoni kutakiwa kuanza kuripoti leo huku kukiwepo na tetesi kuwa itakuwa nje nchi. 
eatv imemtafuta msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ili kuweka wazi hili lakini amesema bado muda wa kuweka wazi kambi yao itawekwa wapi haujafika lakini kwasasa wachezaji wanaendelea na taratibu za kuripoti tu kutoka katika mapumziko waliyopewa na benchi la ufundi.

''Tutaweka wazi tukikamilisha mipango ya kambi yetu, kwasasa bado tunaendelea na maandalizi yanayoanza na wachezaji kuripoti na baada ya hapo tutasema ni eneo gani tutaweka kambi'', - amesema.

Aidha kuhusu tetesi za timu hiyo kuweka kambi nje ya nchi, Manara amesema lolote linawezekana na inaweza ikawa hapa nyumbani ama nje ya nchi lakini kwasasa bado haijajulikana itakuwa wapi.

Kambi za muda mrefu za Simba msimu uliopita katika kujiandaa na mashindano mbalimbali ikiwemo ligi kuu na mechi za kombe la shirikisho barani Afrika, zilikuwa zinafanyika mkoani Morogoro.
 

No comments

Powered by Blogger.