Full-Width Version (true/false)


Mapendekezo ya sheria ndogo ndogo yazua taharuki Songea

 

Manispaa ya Songea  imetoa mapendekezo ya rasimu ya sheria ndogo ndogo yakiwemo tozo za shilingi  laki nne kwa mwaka  kwa taasisi za kidini, na mchango wa shilingi elfu kumi kwa mwaka kwa kila mwananchi hatua inayotafsiriwa na wananchi kurejeshwa kwa kodi ya kichwa kwa mlango wa nyuma. 

Hatua hiyo imezua  mjadala  mkali katika manispaa ya Songea ambapo matangazo ya rasimu hiyo yamebandikwa kwenye mbao za matangazo na wananchi wanatakiwa kutoa maoni yao ndani ya siku kumi na  nne kabla  ya kupitishwa kuwa  sheria kamili. 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololeti Mgema amesema kuwa  wananchi bado wana nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu mapendekezo hayo ili  yafanyiwe marekebisho huku akisema hiyo si kodi ya kichwa. Meya wa manispaa ya Songea  Mstahiki   Abdul  Mshaweji   alipotafutwa   ili alizungumzie suala hilo kwa simu yake ya mkononi  alisema yuko kwenye kikao na alipotafutwa siku ya pili alisema yuko nyumbani kwake  anajisikia  vibaya

No comments

Powered by Blogger.