Full-Width Version (true/false)


Masanduku 209 ya sampuli za madini mbalimbali zakamatwa Madaba Ruvuma.Naibu Waziri wa Madini, Mh. Dotto Biteko amekamata masanduku 209 yakiwa na shehena ya sampuli za madini mbalimbali na kuchwa nyumbani kwa mkazi mmoja wa halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma, Bw. Allan Mbilinyi ambaye anadai sampuli hizo zilikuwa zikihifadhiwa nyumbani kwake na watu kutoka kampuni moja ya Sinohydro iliyokua ikitati masuala ya uwekezaji wa nishati ya umeme katika halmashauri hiyo. 

Sampuli hizo za madini zikiwa zimechwa katika kijiji hiki cha Mtepa-Madaba mkoani Ruvuma nyumbani kwa mkazi mmoja bw. Allan Mbilinyi maarufu kwa jina la Paradiso, ambaye naye ameamua kuanika ngoma juani baada ya wahusika kushindwa kumlipa fedha ya kulinda madini hayo tangu mwaka 2014. 

Maamuzi ya Naibu Waziri wa Madini, Mh. Dotto Biteko ikawa ni kuyasalimisha madini hayo mikononi mwa Mkuu wa wilaya ya Songea, Bw. Pololeti Kamando Mgema ili baadaye yaweze kukishwa kwa wakala wa Gioligia Tanzania (GST) kwa uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia wahusika ili waweze kuchukuliwa hatua.

No comments

Powered by Blogger.