Full-Width Version (true/false)


Mashabiki Simba wamzomea Fei Toto uwanja wa taifa....Feisal Salum Ab­dallah ‘Fei Toto’ amekutana na wakati mgumu wakati mashabiki wa Simba walipomzomea.

Mashabiki wa Simba walimzomea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati akiitumikia timu yake ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Fei Toto alikuwa akiitumikia JKU katika mechi ya Kombe la Kagame kuwania kupata mshindi wa tatu.

Lakini mashabiki wa Simba walikuwa wakimzomea kwa nguvu kila aliposhika mpira.

Mashabiki hao walikuwa uwanjani wakati wakisubiri mechi ya fainali, Simba ikisubiri kuivaa Azam FC ambayo ndiyo kinara kwa maana ya bingwa mtetezi.

No comments

Powered by Blogger.