Full-Width Version (true/false)


Mbao yamnasa MkoreaMbao FC imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili beki wa kulia, Karim Hamim ‘Mkorea’ kwa mkopo kutoka Azam FC.

Tayari timu hiyo ya Jijini Mwanza imeshawatangaza wachezaji watatu wapya iliyowasajili ambao ni Elias Zamfuko (African Lyon), Peter Mwangosi (Njombe Mji) na Emanuel Mtumbuka kutoka Dodoma FC.

Mwenyeki wa klabu hiyo, Solly Njashi alisema usajili huo ni mapendekezo ya benchi la ufundi kuhakikisha timu inafanya vizuri msimu ujao na kwamba uongozi umejipanga kutekeleza.

Alisema wanachotaka ni kuona Mbao ikifanya vizuri na ndio maana kila mchezaji anayetua klabuni humo anakula mkataba wa kuanzia miaka miwili na kuendelea.

“Usajili huu ni mapendekezo ya Benchi la Ufundi kwahiyo sisi uongozi tunachofanya ni utekelezaji,tunataka Mbao endelevu si ya kuishia hapa na ndio maana kila mchezaji anasaini kuanzia miaka miwili,” alisema Njashi.
Kocha wa timu hiyo, Amri Said ‘Stam’ alisema kwa kasi waliyonayo wadau na wapenzi wa timu hiyo watarajie furaha kwani mambo yanaenda vizuri.

Alisema kuwa mipango yake Ligi itakapoanza anahitaji mechi kumi za awali asipoteze mchezo hata mmoja ili kumrahishia nyakati za mwisho kufanya mahesabu.

 “Hadi sasa mambo yanaenda vizuri na bahati nzuri uongozi naona haulali wana kasi ambayo inanivutia na mipango yangu Ligi itakapoanza zile mechi kumi za mwanzo ni kushinda zote,” alisema Kocha Stam.

No comments

Powered by Blogger.