Full-Width Version (true/false)


Mchekeshaji Dullavani achaguliwa kupewa tuzo MarekaniMchekeshaji aliyejizolea umaarufu nchini kupitia uigizaji wake kama mwanamke katika mitandao ya kijamii, Abdallah Sultan ‘Dullavani’ amechaguliwa kushiriki katika tuzo za ‘Go Fun The World’ zilizo andaliwa na ‘9GAG’ zinazo wahusisha waigizaji wa vichekesho wenye ushawishi kwenye mitandao. Akizungumza na eatv Dullavani amesema kuwa mashindano hayo yanayofanyikia nchini Marekani, yameandaliwa kwa dhumuni la kukusanya 'video' fupi zinazofanya vizuri kwenye chaneli za ‘Youtube’ zenye watazamaji wengi ambapo video yake iliyopendekezwa ina watazamaji zaidi ya milioni saba na mshindi atapatiwa dollar lako moja.

“Mimi kila siku nafanya vitu tofauti, na mimi kwenye kazi zangu nazingatia sana ubunifu ndiyo maana hadi leo hii nimepata fursa ya kuchaguliwa kwenye mashindano makubwa duniani na naamini hiyo yote ni kuonyesha niko tofauti na wasanii wengine”, amesema Dullavan.

Ameongeza kuwa wasanii wengi siyo wabunifu na wamekuwa wakifanya sanaa kwa kufanya kazi chini ya kiwango ndiyo maana wanashindwa kuipaisha bendera ya nchi Kimataifa.
 

No comments

Powered by Blogger.