Full-Width Version (true/false)


Mchezaji Yanga akosoa maandalizi ya kikosi dhidi ya Gor mahia CAFWakati Yanga ikiwasili salama huko Nairobi jana, mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Ally Mayay amesema kikosi hicho kimeenda bila maandalizi ya kutosha.
Mayay ameeleza kuwa Yanga imefanya maandalizi ambayo hayaridhishi kwa ajili ya mchezo huo ambao ni wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Julai 18 2018 dhidi ya Gor Mahia FC.
Mayay ambaye ni Mchambuzi wa Masuala ya Soka hivi sasa, amesema Yanga imeenda Nairobi bila kuyapa uzito mashindano hayo kutokana na mechi za kirafiki ilizocheza kutoenda sawa na ukubwa wa mchezo huo dhidi ya Gor Mahia.
Mchezaji huyo wa zamani ndani ya Yanga, anaamini utakuwa ni mchezo mgumu kwakuwa timu haijakaa sawa na imeuchukulia mchezo huo kama wa kawaida akisema kwa namna moja ama nyingine itawapa Yanga changamoto kubwa.
Katika michuano ya KAGAME iliyomalizika wiki jana jijini Dar es Salaam, Mayay amewaelezea Gor Mahia kuwa wameimarika zaidi akisema watakuwa na moto walioondoka nao kwenye mashindano hayo tofauti na Yanga waliocheza michezo ya kirafiki ya kawaida.
"Yanga imeend bila maandalizi ya kutosha, ukiangalia mechi za kirafiki walizocheza haziendani na uzito wa mechi hiyo. Gor Mahia wameondoka kushiriki KAGAME hivyo wataingia kucheza wakiwa wako vizuri zaidi ya Yanga ambao itakuwa changamoto kwao" alisema.

No comments

Powered by Blogger.