Full-Width Version (true/false)


Mchezo wa Mpira Umekuwa kwa Kasi, Azam Ndio Bingwa
Mabingwa wa CECAFA msimu huu Azam Sports Football Club, wamejinadi na kujisifu kuwa wao kuwa mabingwa ni kipimo tosha cha wao kuelekea ligi kuu kutokana na wao kuwafunga bigwa wa zanzibar, Bingwa wa Kenya ambae ndio bingwa wa mabingwa Afrika mashariki, Gor Mahia, wakaendelea kuwafunga Bingwa wa Uganda Viper, na jana kufanikiwa kumpiga bingwa wa Tanzania Simba SC ambapo meneja wa timu hiyo ya azam amesema ni mbaya sana na kusema kuwa wanapoelekea sio padogo wamelenga mbali, hayo yameswemwa na Philip Alando katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini dar es salaam.


Kwa upande wake afisa habari wa Timu hiyo Bw. Jaffar Idd amesema kuwa kombe la kagame wamelichukua mara ya pili mfululizo na kusema kuwa watakapolichukua mara ya tatu kombe litakuwa la kwao, na kuendelea kusema kuwa kombe la kagame litakuwa gumu sana katika msimu ujao sababu hakuna timu itakayokubali azamu wachukue kombe hilo kwa mara nyingine hivyo mechi itakuwa ngumu sana.

Ameendelea kusema kuwa wamepokea salamu kutoka ikulu ambapo Greyson msigwa amewapa pongezi kwa kuchukua kombe hilo kwa mara mbili mfululizo vile vile spika wa bunge Mh. Job Ndugai amewapa pongezi kufuatia ushindi huo walioutwaa dhidi ya Simba SC.

Afisa habari wa Timu hiyo ameendelea Kusisitiza kudai kuwa mchezo wa mpira Tanzania umekuwa sana kutokana na timu zote zilizoingia fainali ni Timu kutoka Tanzania ambazo ni Azam Fc na Simba SC. 

No comments

Powered by Blogger.