Full-Width Version (true/false)


Mfanyakazi wa Ndani Atiwa Mbaroni Kwa Wizi wa Mtoto wa Bosi Wake


Na, magdalena kashindye
Jeshi la polisi Mkoa wa shinyanga linamshikilia binti wa miaka 20 Habiba Abubakari kwa wizi wa mtoto.
 
Katika taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa huo Simon Haule inasema walipata taarifa za kupotea kwa mtoto William Emmanuel kutoka kwa Jeshi la polisi singida.

Taarifa hiyo inaeleza binti huyo aliyekuwa msichana wa kazi za ndani 'House Girl'  wa Hawa Rojas miaka 20 alimuacha mtoto na binti wa kazi na kwenda kwenye shughuli zake na aliporudi nyumbani alimkosa binti huyo na alitoa taarifa kituo cha polisi na juhudi za kumtafuta ziliendelea.

Julai 13, 2018 binti huyo alikamatwa kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga na baada ya kuhojiwa alikiri kutenda kosa hilo na kueleza sababu ya kufanya hivyo ni ugumba uliopelekea kuachana na mumewe Yohana Cyprian (24)

Haule amesema binti huyo atasafirishwa hadi mkoani singida lilipotokea tukio hilo na kuwataka wazazi kuwa makini na watoto wao.

No comments

Powered by Blogger.