Full-Width Version (true/false)


Ukaribu wa Rais wa Croatia na Ufaransa wazua gumzo duniani

Michuano ya kombe la dunia imemalizika wikiendi iliyopita nchini Urusi baada ya kushuhudia timu ya taifa ya Ufaransa ikiibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4 – 2 dhidi ya Croatia.Licha ya ukubwa wa mechi hiyo lakini kinachoendelea kuzungumzwa ni namna rais wa Croatia, Kolinda Grabar Kitarovic alivyokuwa karibu mno na rais Ufaransa, Emmanuel Macron huku wakionekana kama wapenzi hali iliyokuwa kivutio kikubwa machoni mwa wafuatiliaji wa fainali hiyo.Rais huyo wa Croatia, Kolinda Grabar Kitarovic ameitawala myoyo ya watu wengi kufuatia tukio hilo kwenye mchezo wa fainali jijini Moscow hali inayopelekea watu wengi kwenyemitandao kutamani kuona wawili hao wakiwa kwenye mahusiano.Wakati mchezo huo ukiendelea wengi walidhani Kolinda ni Mke wa rais huyo wa Ufaransa, Macron mwenye umri wa miaka 40 ilihali mkewe ni Brigitte mwenye miaka 65.


Kolinda ameolewa na mchambuzi wa maswala ya usalama, Jakov Kitarović tangu mwaka 1996 huku wakiwa wamejaaliwa kupata watoto wawili.

Mama huyo rais wa Croatia alionekana akimkumbatia Macron muda wote na hata wakati wakiwa uwanjani kugawa tuzo wawili hao hawakuhitaji miavuli mvua ilipokuwa ikinyesha.Wengi wameuliza sababu za rais huyo wa Croatia kuwa mwenye furaha muda wote wakati timu yake ikiwa imepoteza dhidi ya Ufaransa je imetokana na taifa lake kutinga fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza au marafiki wakaribu aliyokuwa nao siku hiyo.Grabar Kitarovic ameonekana akiwakumbatia wachezaji wote bila kubagua na kuwapa pongezi kwa kazi nzuri waliyoonyesha uwanjani.Mama huyo mwenye watoto wawili, Grabar Kitarovic amehudhuria michezo yote ambayo taifa lake limecheza isipokuwa moja wa nusu fainali dhidi ya Uingereza kutokana na kuwepo kwenye kikao cha NATO huko Brussels.No comments

Powered by Blogger.