Full-Width Version (true/false)


''Mimi ndio niliamua hivyo'' - Masoud DjumaBaada ya klabu ya soka ya Simba kufungwa mabao 2-1 na Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame hapo jana usiku, kocha wa Simba Masoud Djuma amesema mashabiki hawatakiwi kulalamika kwa kutokuwepo baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza. 


Masoud ameyasema hayo kufuatia baadhi ya mashabiki waliokuwepo uwanjani kuonesha kutoridhishwa na kiwango cha wachezaji waliopewa nafasi ambao wengi wao ni wale waliosajiliwa katika kipindi hiki cha usajili huku wachezaji wazoefu wakiachwa.

''Simba ina wachezaji 30, wengi wao wamecheza ligi na imeisha hawajapumzika ikaja michuano ya SportPesa Super Cup kisha ikaja michuano hii ya CECAFA, mimi nikaamua wapumzike ili warudi kwenye ligi wakiwa vizuri na ninaamini itakuwa hivyo'', - amesema.

Aidha Masoud ameongeza kuwa wachezaji wapya pamoja na wale ambao hawakupata nafasi kwenye ligi msimu uliopita ambao amewatumia kwenye michuano ya CECAFA, wameonesha kiwango kikubwa na sasa anaweza kuamini ana kikosi kipana kwaajili ya michuano mbalimbali msimu ujao.

Endapo Simba ingetwaa ubingwa jana ingekuwa ni mara yake ya 7 kwani tayari ni mabingwa mara 6 wakishikilia rekodi ya kuchukua kombe hilo mara nyingi zaidi. Kwa upande wa Azam FC wao wametetea ubingwa wao ambao waliuchukua mwaka 2015 hivyo kufikisha mara mataji mawili.

Masoud Djuma ambaye ni raia wa Rwanda kwasasa anaifundisha Simba kama kaimu kocha mkuu, baada ya aliyekuwa kocha mkuu Pierre Lechantre kumaliza mkataba na klabu hiyo mapema mwezi Juni na kurejea nyumbani kwao Ufaransa.

No comments

Powered by Blogger.