Full-Width Version (true/false)


Mkandarasi apewa siku 14 Handeni kurudia kazi ya ujenzi vituo vya maji 
Mkuu wa wilaya ya Handeni ametoa siku kumi na nne kwa Mkandarasi alipewa kazi ya kujenga vituo vya kutolea maji ndani ya halmashauri hiyo kurudia kazi na hiyo imetokana  na baadhi ya vituo hivyo kuvijenga chini ya kiwango. 
 
Mkuu huyo ameyasema hayo baada ya kutembelea mradi wa maji uliopo ndani ya halmashauri ya mji wa Handeni huku akiambatana na mbunge wa jimbo la Handeni mjini Mhe. Omari Kigoda na mkuu huyo alianza kwa kuwaonya wakandarasi waliopewa kazi za miradi wilayani hapa kuhakikisha wanazifanya  kulingana na thamani ya fedha wanazo lipwa. 
 
Baada ya kuutembelea mradi huo na kugundua mapungufu ndipo akatoa siku kumi na nne kwa mkandarasi kurudia kazi hiyo huku mbunge akisema kuwa watarudi tena kukagua mradi huo. Wilaya ya Handeni ni moja kati ya wilaya zinazo kabiliwa na tatizo la maji hali hiyo imeacha viongozi mbalimbali wilayani hapa kukagua mara kwa mara miradi ya maji ambayo itasaidia wananchi kuondokana na adha wanayoipata.

No comments

Powered by Blogger.