Full-Width Version (true/false)


Mke wa Barack Obama na mama mzazi wa Beyonce wamwaga radhi Ufaransa kwenye show ya OTR-II (+video)Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama ‘Michelle Obama’ usiku wa Jumapili kuamkia jana akiwa na mama mzazi wa msanii wa Muziki, Beyonce ‘Tina Knowles’ ni moja ya watu maarufu waliohudhuria kwenye show ya OTR-II ya Beyonce na Jay-Z mjini Paris, Ufaransa.
Kitu pekee kilichozua mjadala sio watu hao kuhudhuria kwenye tamasha hilo bali ni kitendo cha wawili hao kucheza mbele ya maelfu ya watu waliohudhuria kwenye show hiyo..

Kwa mujibu wa video zinazosambaa mitandao Michele Obama alionekana mtu mwenye mzuka zaidi kwenye show hiyo kwani licha ya mama Beyonce kuchoka kucheza na kukaa chini mke wa Obama aliendelea kucheza.

Kwenye tamasha hilo mke wa Obama aliongozana na watoto wake Sasha na Malia na baada ya kuanza kucheza watu wengi walianza kumtizama na kumrekodi video kwa njia ya simu.

Hata hivyo, kwenye tamasha hilo Barack Obama hakuwepo alikuwa nchini Kenya kwenye ziara yake ya kikazi. Tayari mamia ya watu mitandaoni wamelaani kitendo hicho cha Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama kucheza hadharani wakidai kuwa amejivunjia heshima.

Wadau wengine wameenda mbali zaidi kwa kudai kudai kuwa hata mavazi aliyokuwa amevaa yalikuwa ni mafupi na hayakuleta picha nzuri kwa watu waliokuwa wanamzunguuka.

Michelle Obama alikaa siku 8 na mumewe Obama nchini Tanzania kabla ya wawili hao kuachana Jumapili Obama akienda Kenya kikazi na Michelle na watoto wao wakienda Ufaransa.

No comments

Powered by Blogger.