Full-Width Version (true/false)


Mkongo aitosa Simba atimkia RwandaKiungo Mkongomani Kakule Fabrice ameitosa Simba na kurudi kwao ili kwenda kumalizana na mabosi wake wa Kiyovu.
Fabrice aliyetua nchini wiki mbili zilizopita ili kufanya majaribio na kama akifanya vizuri ajiunge na timu, lakini mabosi wa Simba wameshtukia kusikia kumbe ana mkataba na klabu yake ya zamani na aliondoka vema huko kwao.

Kiungo huyo aliyewahi kufundishwa na Kocha wa Simba, Masoud Djuma wakati akiwa Rayon Sports aliondoka usiku wa juzi Jumamosi ili kwenda kuweka mambo sawa na kama utamkubalia na mabosi wake arudi na barua la sivyo ndio basi.

“Unajua Fabrice alipendekezwa na kocha Djuma akitaka asaini moja kwa moja, ila tuliomba afanye mazoezi ili amuangalie vizuri maana kama kumfundisha ilikuwa siku nyingi kipindi wapo Rayon,” mmoja wa vigogo wa usajili wa Simba alisema.

“Tukiwa tunamuangalia ndipo zikaja taarifa kwamba hakuondoka vema kwao, kwani bado ana mkataba wa miaka miwili na tusingemsajili mpaka akamalizane na uongozi wake ili kuepuka shida kutoka CAF au FIFA,” alisema.

Hata hivyo, kuondoka kwa Fabrice huenda ndio ikawa kimoja kwani tayari Simba imemsainisha kiungo toka Mtibwa Sugar, Hassani Dilunga huku ikiwa na vifaa wengine katika nafasi hiyo licha ya ukweli kiungo ni fundi kwelikweli.

No comments

Powered by Blogger.