Full-Width Version (true/false)


Mkude kampeleka Feisal Yanga
KAMA angekuwa anataka fedha, basi kiungo Feisal Salum angesaini Simba kwani walishamwekea mezani Sh35 milioni, lakini kiu yake ya kutaka kuvaana na viungo wa timu hiyo akiwamo Jonas Mkude ndio iliyomfanya asaini Jangwani aichezee Yanga.
Akizungumza na Mwanaspoti Feisal alisema wakati akiwa Zanzibar alikuwa akifuatilia kila kitu kuhusu usajili wa Simba na timu yao na kugundua Wekundu hao wana viungo wengi katika nafasi anayocheza, hivyo kuikacha ofa yao.
Feisal alisema aliamua kuikacha ofa hiyo ya Simba na kutua Yanga ili kwenda kupambana na viungo hao wa Simba akiwemo Mkude kuthibitisha ubora wake.
Alisema kwa sasa anatuliza akili yake kabla ya kuja kuungana na Yanga ambapo atahakikisha anathibitisha ubora wake kwa kuisaidia timu yake mpya kukabiliana na viungo wa timu pinzani.
“Sikuja Bara kujiunga na timu yenye fedha nyingi, kama ingekuwa hivyo ningesaini Simba basi, sikutaka kujiunga nao kutokana na nafasi ninayocheza wana viungo wengi sana, lakini mi sipendi kucheza na wachezaji wenye majina makubwa,” alisema.
“Napenda kushindana zaidi na timu zenye majina makubwa nikikabiliana nao hasa timu kama hii Simba ngoja tukutane na hao viungo wao mtaona.”

No comments

Powered by Blogger.