Full-Width Version (true/false)


Moto umewaka msimbazi, Okwi sasa aungana na KagereMshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, amerejea nchini na tayari ameshajiunga na wachezaji wenzake kujinoa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Okwi alisafiri kwenda Uganda kwa ajili ya mapumziko baada ya msimu wa Ligi Kuu 2017/18 kumalizika kutokana na uongozi klabu kutoka likizo kwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza.

Ujio wa Okwi unakuwa unakutanisha na straika mpya hatari aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka Gor Mahia FC ya Kenya, Meddie Kagere, ambaye alianza kutema cheche zake katika mashindano ya KAGAME.

Mbali na Kagere, Okwi atakuwa anacheza sambamba na Adam Salamba pamoja na Marcel Kaheza ambao pia wamesajiliwa baada ya msimu wa ligi kumalizika na kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya.

Kikosi cha Simba kimekuwa na ratiba ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya jijini Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Uwanja wa Boko Vetrani.

No comments

Powered by Blogger.