Full-Width Version (true/false)


Mrembo aivuruga ndoa ya Uwoya na Dogo JanjaNDOA staa wa filamu Bongo Muvi, Irene Iwoya na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ imedaiwa kupigwa ‘kombora’ la aina yake baada ya mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Dayana kuwa na mawasiliano ‘hatarishi’ na Dogo Janja ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake.

Ijumaa Wikienda lilitonywa kuwa, Uwoya na Dogo Janja hawako sawa baada ya muigizaji huyo kushtukia mchezo mchafu wa mumewe na Dayana.

“Fuatilieni, Uwoya na Dogo Janja hawako sawa kabisa chanzo ni Dayana, nasikia wanawasiliana sana na mara kadhaa Dogo Janja ameshindwa kuvumilia hadi kumposti kimafumbo kwenye ukurasa wake wa Istagram,” kilieleza chanzo makini.

Baada ya kutonywa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilianza kumsaka Dayana ili aweze kufungukia madai ya kuwa chanzo cha kuitikisa ndoa ya Uwoya ambapo alipopatikana, hakutaka kukubali wala kukataa kama ‘anabanjuka’ na Dogo Janja zaidi akamshauri Uwoya amtulize mumewe akidai bado ni kijana mdogo.

“Ningepanda sana kumshauri dada yangu Uwoya kuwa kwanza amsihi mumewe asiwe ananisumbua kwa simu kwa sababu mimi niko na mtu mwingine lakini najua atapata naye tabu sana kwa sababu Dogo Janja bado mdogo hivyo bado hajafika kwenye safari ya mapenzi,” alisema Dayana.

Akiendeleza kuchezesha taya na Ijumaa Wikienda, Dayana alisema, anatamani Uwoya angepata mtu ambaye wanaendana kiumri kwa sababu hatampa tabu na hatakuwa na mambo mengi ya ujana lakini sio kwa Dogo Janja ambaye bado damu inachemka. “Nafikiri ingekuwa vizuri kabisa Uwoya angemtafuta mtu ambaye analingana naye lakini hivi sio sawa atapata tabu sana ni bora kuwa na mtu mzima mwenzake,” alisema Dayana.

Baada ya gazeti hili kuzungumza na Dayana, lilimtafuta Uwoya ili kusikia anamzungumziaje ‘mwizi’ wake ambaye pia amempa ushauri ambapo alipopatikana hakutaka kufunguka kwa kirefu zaidi ya kusema amepokea ushauri wake.

“Sidhani kama kuna kitu kikubwa cha kusema ila tu nashukuru ushauri wake nimeupokea nitaufanyia kazi,” alisema Uwoya. Kwa upande wake Dogo Janja alipotafutwa ili kuweza kumsikia anazunguziaje ishu hiyo, simu yake haikuwa hewani. Jitihada za kumtafuta zinaendelea.

No comments

Powered by Blogger.