Full-Width Version (true/false)


Msanii maarufu nchini Kenya Alilia Penzi la Wema Sepetu

Msanii wa muziki maarufu nchini Kenya, Brown Mauzo ametangaza wazi kuwa kwa namna na hali yoyote ile yupo tayari kumuoa mrembo Wema Sepetu.

Brown amesema kuwa amekuwa akivutiwa sana na Wema Sepetu na yupo tayari muda wowote kumuoa mrembo huyo hata kama ikibidi awe spea tairi.

Akifunguka kupitia kipindi cha eNEWS cha EATV Brown amesema; “Mimi namzimia sana Wema Sepetu kwa bahati mbaya sijawahi kuonana naye namzimiaga sana.

"Kila mtu anasema ukweli kutoka moyoni kila shetani na mbuyu wake. Licha ya kwamba alikuwa na nani sijui na nani ila mimi nipo tayari kumuoa, na popote atakapokuwa namwambia mimi nampenda na nataka kumuoa.. hata kama akiwa na mtu mwingine mimi nipo tayari hata niwe spea tairi,”.

Kwa upande mwingine Brown amesema kuwa Wema Sepetu ni mwanamke mwenye sifa zote anazozitaka na ikiwezekana hata kesho yeye yupo tayari kufunga naye ndoa.

Brown Mauzo alishawahi kufanya ngoma na Alikiba iliyokwenda kwa jina la Nitulize na kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya Zagada.

No comments

Powered by Blogger.