Full-Width Version (true/false)


Mtanzania aliyedaiwa kupata ugonjwa wa kichaa Sauz, ndugu zake wapatikana.Hivi karibuni taarifa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii  kuhusu Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Gabriel, lakini jina lake halisi ni (Paul Joseph Tesha), mkazi wa Mbagala jijini Dar ambaye ilidaiwa alipatwa na ugonjwa wa kichaa akiwa nchini Afrika Kusini baada ya mwenyeji wake aliyemfuata nchini humo kumzimia simu, lakini leo ndugu zake wamepatikana.

Mama wa Mtanzania huyo, Restuta Mwamba amesema 

 ’’Mtoto wangu aliondoka nyumbani miaka mitano iliyopita, alitoroka alfajiri, nilimtafuta sana bila mafanikio, sikuwa na mawasiliano naye, baba yake alifariki miaka miwili iliyopita hajamzika, hii ni mara ya pili kwenda Sauz alirudishwa na serikali lakini alionekana hana furaha alikuwa akikaa peke yake kama mtu aliyezubaa, sio mchangamfu kama zamani tuliamua kumpeleka hospitali ya Temeke alipimwa alionekana hana tatizo lolote daktari alisema ana msongo wa mawazo alipewa matibabu akawa anahudhulia kliniki’’ 

Amesema wanaiomba serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kumrudisha nchini kwani hawana uwezo wa kumrudisha hapa nchini.

No comments

Powered by Blogger.