Full-Width Version (true/false)


Mtawakoma Mbao FC washusha silaha mbili
Mwanza. Mbao FC imekamilisha usajili wa nyota wawili mshambuliaji Emanuel Mtumbuka na beki wa kati, Peter Mwangosi ikiwa

Usajili huo wa kwanza kwa timu hiyo kwa wachezaji wapya tangu kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili kwa klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na la Pili.

Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi alithibitisha kuwanasa nyota hao kutoka timu tofauti na kwamba kila mmoja amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Mbao FC.

Alisema Mtumbuka (Emanuel) amenaswa kutoka Dodoma FC na beki wa kati Mwangosi (Peter) kutoka Njombe Mji iliyoshuka daraja msimu uliopita.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mpango wao ni kusajili wachezaji saba, hivyo mazungumzo kwa nyota wengine watano yanaendelea na muda wowote watamalizana nao.
Alisema uongozi umejipanga vizuri kuhakikisha wanasajili wachezaji wenye uwezo ambao wataweza kuitumikia timu kwa mafanikio.

No comments

Powered by Blogger.