Full-Width Version (true/false)


Mtibwa Sugar yaingia kandarasi na Juma LiuzioMabingwa wapya wa michuano ya Azam Sports Federation Cup Mtibwa Sugar hii leo wamefanikiwa kumsajili mchezaji, Juma Liuzio.

Mtibwa wamemsajili, Liuzio baada ya kumaliza mkataba wake wa kuitumikia mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba.

Luizio aliwahi kuitumikia timu ya vijana ya Mtibwa Sugar kabla ya kutimkia Zambia alipoichezea  klabu ya Zesco na baadae kurejea tena nchini.

No comments

Powered by Blogger.